Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Isitu Wilayani Mbarali, Geofrey Emilio Mwanganga(21) kwa kumuua mtoto wake, Prince Geofrey Emilio(5)
Mtuhumiwa anadaiwa kumuua mwanae kwa kumnywesha sumu (haijafahamika aina yake) na kisha Agosti 28, baba huyo
alikwenda nyumbani kwa mkewe alikokuwa anaishi baada ya kutengana na kumchukua mtoto huyo kwa nguvu bila kibali cha mzazi mwenzake
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa, alidai mtoto alikuwa amempeleka kwa ndugu zake huko Makete Mkoani Njombe lakini baadae alikiri kuwa amemuua mtoto na kumtupa porini
Aidha, chanzo cha tukio hili ni mtuhumiwa kuhisi mtoto (marehemu) si wake bali amebambikiwa mtoto wa mwanaume mwinginewenda kumfukia porini
Comments
Post a Comment