Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Bashiru Ally atuma salamu za rambirambi ajali MV Nyerere



Mtwara. Katibu Mkuu waCCM Dk Bashiru Ally ametuma salamu za rambirambi kwa Rais John Magufuli na Watanzania kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi Septemba 20, 2018 Kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza.
Ametuma salamu hizo leo Jumamosi Septemba 22, 2018 akiwa mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi, kulazimika kubadili ratiba ya ziara hiyo.
“Taifa letu lipo kwenye msiba na kama mnavyojua bendera zinapepea nusu mlingoti. Tuendelee kuwaombea na tutafakari namna tunavyoweza kukabiliana na majanga yanayotokea,”amesema Dk Bashiru.
“Tupate fursa ya kutafakari na kujadiliana namna nzuri ya kusimamia vyombo vyetu vya usafiri na shughuli zote zinazohusu huduma kwa Watanzania.”
Amesema kutokana na ajali hiyo amelazimika kubadili ratiba ya ziara yake na kuungana na Watanzania wengine katika maombolezo.
 “Sijasitisha  ziara yangu lakini itabidi baadhi ya ratiba zirekebishwe ziendane na maombolezo,” amesema.
“Nimewatuma wajumbe wawili Humphrey Polepole (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) na  Kanali Lubinga (Ngemela-Katibu wa Siasa na Uhuasiano wa Kimataifa wa CCM) kwenda kule wafuatilie  namna shughuli zinavyoedelea.”

Comments

Popular Posts