Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kagame, Uhuru watoa pole kupitia akaunti zao za twitter

Rais  Paul Kagame wa Rwanda(kushoto) na Rais 

Rais  Paul Kagame wa Rwanda(kushoto) na Rais  Uhuru Kenyatta wa Kenya
Dar es Salaam. Salamu za rambirambi kufuatia kuzama kwa Kivuko cha Mv Nyerere zimeendelea kumiminika kutoka ndani na nje ya nchi.
Jana kupitia akaunti zao za twitter, marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda katika nyakati tofauti wali-tweet wakisema mataifa yao yapo pamoja na waombolezaji katika msiba huo mkubwa.
Walisema wanaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Rais Uhuru aliandika, “Wakenya wako pamoja na ndugu zao Watanzania katika kipindi hiki kigumu.”
Salamu hizo amemtumia Rais John Magufuli na kusisitiza kuwa hana maneno yanayotosha kuielezea ajali hiyo.
Bali anawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani na majeruhi, Mungu awajalie uponyaji wa haraka.
Naye Rais Kagame katika akaunti yake ya twitter ameandika, “Pole zetu nyingi sana kwa familia na wapendwa wa waathirika wa ajali ya kivuko cha Ziwa Victoria, tupo pamoja nanyi.”

Comments

Popular Posts