Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kifo cha profesa chuo cha Muhimbili chazua utata



Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Muhas), Emil Kikwilu amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya mwili wake kukutwa karibu na nyumbani kwake ukiwa na majeraha kichwani.
Msemaji wa familia ya marehemu, Zenodi Shauritanga leo Jumamosi Septemba Mosi, kuwa mwili wa msomi huyo  uliokotwa Agosti 27, 2018 ukiwa hatua 15 kutoka nyumbani kwake.
Mwili wa Profesa huyo uliagwa katika viwanja vya chuo hicho jana Agosti 31, 2018 na kuzikwa nje ya nyumba yake, Kimara jijini Dar es Salaam.
“Tuliona mwili kati ya saa tatu usiku wa siku hiyo, ulikuwa na majeraha makubwa kichwani ni kama vile alikatwa,” amesema Shauritanga.
“Niliitwa na kushuhudia na baadaye polisi walifika wakauchukua mwili na kuupeleka mochwari katika hospitali ya Taifa Muhimbili.”
Amesema alifariki dunia wakati akirejea nyumbani akitokea kazini, kwamba hakukutwa na simu, begi alilokuwa akiweka kompyuta mpakato na vyombo vyake alivyokuwa akiweka chakula.
“Tulikuta mwili kwenye kichochoro sehemu ambayo gari wala pikipiki haviwezi kupita. Hatujui kilitokea nini tunasubiri taarifa za uchunguzi wa polisi,” amesema Shauritanga.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema walipata taarifa kuhusu tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi kwa kuwa kifo hicho kina utata.
"Tunachunguza ili kujua sababu za kifo chake, tukikamilisha tutaijulisha familia yake," amesema.

Comments