Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Lukuvi apiga marufuku kampuni binafsi kupima ardhi


Serikali imepiga marufuku kampuni binafisi za upimaji ardhi ambazo zimekuwa zikiingia makubaliano ya upimaji ardhi za wananachi bila hata uongozi wa Wilaya husika kuwa na taarifa.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya wakazi wa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora kuilalamikia Kampuni ya Ardhi Plan kuwachangisha fedha zao bila ya kupimia ardhi yao.
Amsema kuanzia sasa nchini kote hakuna Kampuni binafsi ya aina yoyote inaruhusiwa kwenda na kuingia moja kwa moja makubaliano na wananchi ya kuwapimia maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya husika.
Lukuvi amesema kuwa Kampuni za aina hiyo zimekuwa zikiwachangisha fedha na kugawana mapato bila hata ya kuwapimia wananchi huku uongozi wa Wilaya husika ukiwa hauna hata taarifa.
Aidha, amesema haiwezekani upimaji wa ardhi za wanyonge ukageuza uchochoro wa kuwaibia na kuwadhulumu wananachi haki zao na kuongeza kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe katika upimaji wa ardhi za wananchi na taarifa ziwe kwa Wakuu wa Wilaya.
Hata hivyo, Lukuvi amezitaka halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia Chuo cha Ardhi Tabora na kuachana na Kampuni za nje kupima ardhi ili kuepuka matumizi makubwa ya gharama za zoezi hilo.

Comments

Popular Posts