Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Madiwani ACT Wazalendo, Chadema wajiunga CCM



Misungwi. Madiwani wawili wa Chadema na ACT Wazalendo wilayani Misungwi jijini Mwanza  wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na CCM.
Madiwani hao ni Marco Kadala wa (Buhingo-Chadema) na Isanzu Elikana wa  Sumbugu kupitia ACT Wazalendo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Kisena Mabuba amethibitisha kupokea barua za madiwani hao kujiuzulu  Septemba 18,2018.
Amesema kisheria taarifa zimekwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kupanga uchaguzi mdogo kwenye kata hizo.
Kadala amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuona jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli kwenye shughuli za maendeleo na kudhibiti fedha za Serikali kwa kuwakamata wabadhirifu.
Naye Elikana amesema amefikia uamuzi huo baada ya CCM kujisafisha na kuwa mpya.
Kaimu katibu wa Chadema wilaya ya Misungwi, Mwika Musa amesema kitendo alichokifanya Kadala ni uamuzi wake maana hakukishirikisha chama kilichomfanya kuonekana kuwa mzoefu kwenye baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo wilayani humo, Joseph Nyamwanja amesema Elikana walimpokea kutoka CCM baada ya kushindwa kwenye kura za maoni.
“Tumempa weledi wa kutosha sana na kuchangia hoja ambazo ni nzito, tunamtakia kila la heri huko aendako,” amesema.
Viongozi hao walipokewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kheri James katika kijiji cha Mbele A wilayani hapa jana.

Comments