Baadhi ya wananchi wakiwa katika eneo la Bugorola wakisubiri Feri ya MV Nyehunge ambayo inadaiwa kwamba itafika hapo baada ya masaa mawili.
Ukerewe. Zaidi ya wananchi 500 wamekwama katika eneo la Bugolora baada ya kukosa usafiri wa kuelekea kisiwa cha Ukara kulikotokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018.
Wananchi hao wanaoelekea kisiwani humo kutambua miili ya ndugu zao, wamekosa usafiri kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokwenda Ukara, wakiwemo viongozi mbalimbali wa Serikali.
leo Jumamosi Septemba 22, 2018 wameiomba Serikali kusaka njia mbadala ili kuwasaidia waweze kufika Ukara.
Lucas Makuna mkazi wa jijini Mwanza amesema huenda asiuone mwili wa kaka yake aliyefariki dunia katika ajali hiyo kwa kuwa muda umekwenda na inawekezana zoezi la utambuzi wa miili likawa na changamoto.
“Ninakumbuka mwaka 1996 ilipozama MV Bukoba baadhi ya watu walishindwa kuitambua miili ya jamaa zao hadi Serikali ikaamua kuwazika kwa pamoja,” amesema Makuna.
“Sikutaka hili litokee Serikali iangalie namna MV Nyehunge itafika hapa maana ipo kule Ukara pamoja na MV Clarias sasa sijajua kwanini.”
Christina Mwikwabe ambaye amekwama eneo hilo amesema aliwahi alfajiri katika eneo la Bogolora ili afike Ukara mapema kuutambua mwili wa mtoto wake lakini ameshindwa kufika.
Mariam Nguzu ambaye amekwama kuvuka amesema kivuko cha MV Nyehunge hakina mafuta tangu jana usiku.
Comments
Post a Comment