Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhandisi kivuko cha MV Nyerere akutwa hai majini



Ukerewe. Licha ya kivuko cha Mv Nyerere kuzama majini zaidi ya saa 48 zilizopita wilayani Ukerewe, Alphonce Charahani, mhandisi wa kivuko hicho ameokolewa leo asubuhi akiwa hai.
Kivuko hicho kilizama juzi mchana, lakini Charahani ameokolewa leo Jumamosi Septemba 22, 2018 saa 4:45 asubuhi akiwa hai.
 iliyopo eneo la tukio imeshuhudia mhandisi huyo akitolewa akiwa hai na kukimbizwa Kituo cha Afya cha Busya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara.
 mmoja wa wazamiaji, Daniel Kondoyo amesema tangu juzi Septemba 20, 2018 kilipozama kivuko hicho kila walipokuwa wakigonga walisikia mtu mwingine akigonga kwa ndani.
Baadhi ya wazamiaji wanaoopoa miili wamesema Charahani alikuwa amejipaka oili mwilini ambayo wameielezea kuwa husaidia maji yasiweze kupita katika vinyweleo.
Kandoyo amesema kutokana na hali hiyo huenda aliyekuwa akigonga kwa ndani ni Charahani.

Comments

Popular Posts