Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Rais Magufuli Amcharukia Mbowe.."Usitafute Kiki Kwenye Msimba wa MV Nyerere"


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaonya wanasiasa kutumia tukio la msiba wa jali ya MV Nyerere kutafutia kiki za kisiasa kana kwamba wanafahamu ajali hiyo ilivyotokea.

Magufuli amesema hayo leo jioni wakati akitoa salam za pole kwa Taiofa kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana na kuua jumla ya watu 131 wamepoteza maisha huku wengine 40 wakiokolewa.

Kauli hiyo ya rais imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuzungumza na vyombo vya habari na kumtaka Rais awawajibishe wote waliohusika na tukio hilo huku akiilalamikia serikali kwa madai ya kushindwa kufanya juhudi za uokoaji kwa jana na kusitisha zoezi hilo hadi leo kutokana na giza.

Mbali na Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia naye alitoa kauli akiitaka serikali kuboresha mindombinu ya uokoaji na kutoa elimu hiyo ikiwa ni sambamba na kuanzishwa kwa chombo maalum cha kupambana na maafa.

 Aidha, Rais ameagiza Bendera ya Taifa kupepea nusu mlingoti kwa siku nne kuanzia leo Septemba 21 hadi Septemba 24, kufuatia ajali hiyo na kuagiza wahusika wote wakamatwe na kuhojiwa na watakaokutwa na hatia wachukuliwe hatua.

VIDEO:

Comments

Popular Posts