Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Ummy Mwalimu aongoza mamia matembezi ya Ebola



Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo asubuhi Jumamosi Septemba 22, 2018 ameongeza mamia ya wananchi wa jijini Dar es Salaam katika matembezi ya hiari kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.
Viongozi mbalimbali wameshiriki matembezi hayo wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari Kambi.
Matembezi hayo yameanza saa 1:00 asubuhi katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kupitia barabara ya Palm Beach na baadaye kuzunguka fukwe ya Coco Beach na kuhitimisha matembezi hayo katika ukumbi wa Karimjee saa 2:00 asubuhi.
Walioshiriki matembezi hayo walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka waliofariki katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere, kilichozama Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Comments

Popular Posts