Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Updates: Miili Mingine Mitano Yaopolewa Ajali MV Nyerere.....Waliofariki Dunia Wafika 157

Updates: Miili Mingine Mitano Yaopolewa Ajali MV Nyerere.....Waliofariki Dunia Wafika 157

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157  huku uokoaji ukiendelea.

Akizungumza akiwa katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018.

“Leo miili mingine imeopolewa lakini bado uopoaji unaendelea,” amesema.

Amesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na ikitarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.

“Vikosi vya uokoaji vinafanya kazi yake vizuri na tunaendelea na tunatarajia Mungu akijalia hadi kesho tutakuwa tumekamilisha,” alibainisha mkuu huyo wa mkoa.

Mongella amesema kuwa baadhi ya miili imeshatambuliwa huku kazi ya utambuzi akisema inaendelea.

“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.

Comments

Popular Posts