Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichozama katika eneo la Bwisya, takribani mita 100 kabla ya kufika bandari ya Ukara imefikia 148, huku kazi ya ukoaji likiendelea.
Kivuko hicho kinachofanya safari kwa kusafirisha abiria na mizigo kati ya Ukara na Bugorora wilayani Ukerewe, kilizama juzi majira ya saa 8:10 mchana baada ya kutoka katika bandari ya Bugorora kwenda Ukara.
Kutokana na ajali hiyo, watu 40 pekee ndio waliookolewa wakiwa hai na 136 waliopolewa wakiwa wameshafariki dunia hadi jana jioni.
Leo Septemba 22, 2018 asubuhi Miili mingine 12 imeopolewa na hivyo kufanya miili iliyopatikana hadi sasa kufikia 148.
Comments
Post a Comment