Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Video: Sakata la Makontena ya Makonda Le Mutuz Amuomba Msamaha Waziri Mpango

Sakata la Makontena ya Makonda Le Mutuz Amuomba Msamaha Waziri Mpango

Mjasiriamali ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, john Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz amesema amemuomba msamaha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kufuatia kauli yake kuhusu mkontena ya RC Paul Makonda yaliyokamatwa bandarini kwa kushindwa kuyalipia kodi.

Lemutuz amesema kwa uelewa wake alidhani baada ya makontena hayo kukamatwa, samani zote zilizomo ndani zingepelekwa na kugawiwa mashuleni, lakini baada ya Rais Magufuli kufafanu juzi kwamba mwenye mamlaka ya kupokea misaada ni Waziri wa Fedha pekee, hivyo Lemutuz aliielewa sheria, amemuomba msamaha Waziri na kuiachia serikali ifanye maamuzi.


Comments